Sunday, December 2, 2012

MZEE MAJUTO (a.k.a KING MAJUTO) YUKO JUU NA VITEGA UCHUMI VYAKE

Mfano wa Kuigwa: Usimuone Anavyouza Sura Mjini Ukajua Hajajipanga. Big Up!!!!! Yupo Kikazi Zaidi 

              Hiyo Noah ya kulia anaitumia kutembelea tu ila hizi za kushoto ni daladala za abiria.
 

daladala ya kwanza

 
daladala ya tatu.
.
Hii nyumba ni yake na ndimo anamoishi, hana nyumba Dar es salaam.
.
.
.
.
Mtaa anaoishi.
.
Hii ni sehemu ya familia yake kasoro huyo alievaa nguo ya zambarao, ana
watoto saba ambapo wa kwanza amezaliwa miaka ya 70 na huyo mama ndio mke wake pekee.
 
Taarifa na Milardayo.com

PICHA ZA KUONYESHA TASWIRA NZIMA YA MAZISHI YA SHARO MILIONEA

 
 
  Mwili wa Marehemu Hussein Ramadhan 'Sharo Milionea' ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.…
 
Mazishi ya Sharo Milionea yakiendelea kijijini kwao Lusanga - Muheza, mkoani Tanga.

Sehemu ya umati wa watu walioshiriki mazishi ya Sharo Milionea yaliyofanyika Novemba 28, 2012.
 
Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea, Mzee Majuto akielezea machache kuhusu marehemu.

Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya marehemu Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea' kijijini kwao Lusanga wilayani Muheza mkoani Tanga leo.
 
Waombolezaji waliopoteza fahamu wakipatiwa huduma ya kwanza msibani hapo.
 
Miss Kinondoni namba 2, 2011, Husna Maulid akilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya Sharo Milionea yaliyofanyika Novemba 28, 2012.
Picha Zote kwa hisani ya GPL.
 
Habari na picha zote kwa hisani ya Global Publishers.

Wednesday, November 28, 2012

MSANII SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA TANGA


Msanii maarufu wa filamu na Vichekesho nchini almaarufu kama Sharo Millionea amefariki Dunia Kutokana na Ajali ya Gari  alilokuwa akiendesha aina ya Harrier eneo la Muheza Mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini inasema Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Sharobaro, baada ya kupata ajali majira ya saa 2 usiku katika kijiji cha Lusanga, Muheza ambapo pia ndio nyumbani kwao.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga.
Msanii huyo maarufu ambaye amefanya tangazo la mtandao wa simu za Mkononi wa Airtel pamoja na Tangazo la Kinywaji cha Azam Cola akishirikiana na mwenzake King Majuto  ambayo yamekuwa kivutio kwa watoto na wakubwa kutoka na staili ya kuweka mdomo pembeni akionyesha jinsi gani mashabaro walivyo.
JIMMY CHUMA BLOG: Iko pamoja na Familia ya marehemu sanjari na Watanzania wote  kwa ujumla katika kuomboleza msiba huu mkubwa wa mpendwa wetu Sharo Millionea.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi Amen.

Wananchi wakiangalia gari lililosababisha kifo msanii Sharo Milionea
Marehemu Sharo Milionea (kulia) na Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wao.


Saturday, September 10, 2011

MELI IMEZAMA UNGUJA NA ABIRIA ZAIDI YA 610 WAHOFIWA KUFA ALAFAJIRI YA LEO

Pichani Meli ya LCT Islanders ikiwa imezama Pwani ya Nungwi, Unguja. Picha kwa hisani ya Zanzinet.

Meli ya LCT SPICE ISALNDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Pwani ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati ikielekea Pemba.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Mhe. Haji Issa Ussi akithibitisha tukio hilo amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo ikiwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo. 

Mhe. Ussi amesema kuwa meli hiyo iliondoka Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima kabisa lakini katikati ya safari ikatokea hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama. Hadi sasa bado haijafamika idadi kamili ya watu waliofariki katika ajali hiyo lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio ili kutoa msaada.

 Naibu Waziri huyo amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya usafiri binafsi vya boti ziendazo kasi zimekwenda katika eneo la tukio kutoa msaada unaohitajika, hali kadhalika Jeshi la Polisi limetuma Helikopta yake kwenye eneo la tukio.

 Awali, Mhe Ussi amesema kuwa mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli nyingine ya MV Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo nayo ililazimika kukatisha safari yake ili kuelekea Kisiwa cha Pemba na kwenda kwenye tukio.

Serikali imewaomba wanananchi kuwa watulivu na taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa kuhusiana na ajali hiyo kwa ujumla.

Habari hizi ni kwa Hisani ya Blogu ya Issa Michuzi

Tuesday, September 6, 2011

JOYCE KIRIA AFUNGA NDOA!!!! TENA AU?? WEWE UNAJUA HIYO???

Mtangazaji maarufu wa kituo cha Televisheni cha East Africa Bi. Joyce Kiria amefunga ndoa mapema mwanzoni mwa mwezi huu siku ya jumapili tarehe 04 Septemba, 2011. Ndoa hiyo aliyofunga na Bw. Henry John Kileo ilifuatiwa na hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Atrium iliyopo Sinza jijini Dar.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na waheshimiwa wabunge wa CHADEMA, Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini), Bw. Freeman Mbowe (Hai) na Bw. John Mnyika (Ubungo) pamoja na wadau wengine mbalimbali.

 SINA UHAKIKA ila inasemekana kuwa Bi. Joyce ni mke wa mtu na alishawahi kufunga ndoa (nakumbuka alikuwa anatumia jina la Joyce Kiria Nkongo) lakini sasa hatumii jina hilo na ameolewa na Bw. Henry J. Kileo.
Mimi sio mwanzilishi wa hili ila nimeipata huku, BOFYA HAPA AU ANGALIA HAPA
Bw. Henry J. Kileo akimvisha pete ya ndoa mke wake Bi. Joyce Kiria

Bi. Joyce Kiria akiwa katika pozi la furaha mara baada ya kufunga ndoa.

 Hongera Dada Joyce na Bw. Henry Kileo, Mungu abariki ndoa yenu.

Thursday, September 1, 2011

BENYONCE AONESHA MIMBA YAKE JUKWAANI

Hivi karibuni, mwanamuziki Beyonce Knowles alisimama jukwani wakati akifanya perfomance ya nyimbo zake katika tamasha aliamua kufungua vifungo vya kikoti chake na kuonesha tumbo la mimba yake huku mumewe Jay Z akifurahia kwa pembeni.

 Yamkini Beyonce aliamua kufanya kituko hicho kufuatia uvumi uliokuwa ukienea kwa miaka kadhaa kuwa mwanamuziki huyo ni mjamzito lakini sasa imethibitika kuwa kweli, kama wahenga walivyosema “Lisemwalo lipo na kama halipo laja” na sasa Beyonce ameamua kuweka bayana suala hilo.

 Beyonce ambaye anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mumewe ambaye pia ni Mwanamuziki Jay Z ambapo uzao huo unatarajiwa kuwa ni uzao mwema kwao kwani magazeti mengi ya udaku yamekuwa yakiripoti kimakosa kuhusu Beyonce kuwa ni mjamzito mara kwa mara na kuwachanganya wapenzi wa mwanadada huyo.
Kama kuna jambo moja ambalo linaweza kumlamzimisha mrembo wa R&B kuvaa nguo nyepesi za kisasa na za kawaida, ni wakati wa matarajio ya uzazi kwa akinamama ujauzito), ni furaha sana.
Beyonce akitabasamu kwa washabiki wake huku akiwa ameshikilia tumbo lake.
Ili kuona live video ya kituko hicho cha Beyonce; BOFYA HAPA TARTIIIBU.